Kutokana na hali ya mafuriko
yaliyoikumba Kilosa Mwanzoni mwa mwaka 2016 wafanyakazi wa Wezesha walitembelea
wahanga wa mafuriko na kuweza kuwafariji kwa namna ya tofauti wakiamini kwamba
tatizo la wahanga ni letu sote, hivyo basi walifanikiwa kupeleka misaada ya
vyakula, nguo, pesa taslimu na misaada mbalimbali ili kuhakikisha hata
kile kidogo kilichotolewa kinaweza kuwafuta machozi wahathirika japokuwa
haiwezekani kutatua tatizo hilo kwa mara moja.
Wahanga hawa wameharibikiwa
nyumba zao hawana makazi tena, hawana mashamba tena, makanisa, misikiti na hata
miundo mbinu imeharibika. Tunaiomba jamii kujitoa kwa matukio yoyote
yanayohusu jamii tukiamini kwamba sisi sote ni ndugu na tunatakiwa tukimbiliane
na kusaidiana. Poleni ndugu zetu na poleni wote mlioathirika. Tunaamini Mungu
wetu wa mbinguni atafanya njia hata pasipo na njia.
Kushoto ni aliyekuwa Afisa Tawala wa Wilaya akishukuru misaada kama anavyoonekana pichani.
Wafanyakazi wa Wilaya ya Kilosa, Wezesha na wadau waliohudhuria mapokezi ya misaada hiyo kwa pamoja wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya akitoa shukrani za dhati kwa Asasi ya Wezesha
Mkuu wa
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wakishusha mizigo toka ndani ya gari iliyobeba misaada hiyo.
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund kushoto Mohamed Nyongo na Salum Tingwa wakiingia nyumba iliyoathirika na mafuriko kutathmini athari zilizopatikana.
Wafanyakazi wa Wezesha wakiangalia athari zilizopatikana kwenye mafuriko hayo, ni hali ya hatari kwa kweli watu wengi wamekosa makazi na wamekosa hata mahali pa kujificha kuweza kuendelea na maisha. Serikali imewaahidi kuwaandalia eneo la kuwajengea. Waathirika wanasubiri kama serikali ilivyowahidi.
Wakinama waathirika wakitoka kuchoka maji mbali sana kutokana na athari ya mafuriko. Waliezea hali halisi ya mafuriko hayo kwamba eneo hilo ni hatari hata kwa kuishi kwani mkondo wa maji umepita tangu miaka mingi iliyopita.
Mto Mkondoa, ni mto ambao umemwaga maji na kusababisha mafuriko baada ya kujaa na kingo za mto kuzidiwa kuhifadhi maji na kuyafanya yatiririke mpaka maeneo wanayoishi watu. Serikali tunaomba iweze kulifanyia ukarabati daraja hili kwa manufaa ya wananchi wa Kilosa na waathirika kwa ujumla.
EmoticonEmoticon