ZIARA YA WAFANYAKAZI WA WEZESHA KWA WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA MEI, 2016

1:07 AM
Kutokana na hali ya mafuriko yaliyoikumba Kilosa Mwanzoni mwa mwaka 2016 wafanyakazi wa Wezesha walitembelea wahanga wa mafuriko na kuweza kuwafariji kwa namna ya tofauti wakiamini kwamba tatizo la wahanga ni letu sote, hivyo basi walifanikiwa kupeleka misaada ya vyakula, nguo, pesa taslimu na misaada mbalimbali ili kuhakikisha hata kile kidogo kilichotolewa kinaweza kuwafuta machozi wahathirika japokuwa haiwezekani kutatua tatizo hilo kwa mara moja.  

Wahanga hawa wameharibikiwa nyumba zao hawana makazi tena, hawana mashamba tena, makanisa, misikiti na hata miundo mbinu imeharibika.  Tunaiomba jamii kujitoa kwa matukio yoyote yanayohusu jamii tukiamini kwamba sisi sote ni ndugu na tunatakiwa tukimbiliane na kusaidiana. Poleni ndugu zetu na poleni wote mlioathirika. Tunaamini Mungu wetu wa mbinguni atafanya njia hata pasipo na njia. 


 Mkurugenzi wa Wezesha Trust Fund Bi. Lusako Mwakiluma akikabidhi misaada kwa waathirika wa mafuriko Wilayani Kilosa Mei, 2016 kulia ni  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Henjewele akipokea misaada hiyo: Chakula, Nguo, Pesa taslimu na vitu vingine vingi kama pole kwa Wahanga wa mafuriko hayo.
 Kushoto ni aliyekuwa Afisa Tawala wa Wilaya akishukuru misaada kama anavyoonekana pichani.
 Wafanyakazi wa Wilaya ya Kilosa, Wezesha na wadau waliohudhuria mapokezi ya misaada hiyo kwa pamoja wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya akitoa shukrani za dhati kwa Asasi ya Wezesha
 Mkuu wa
 Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wakishusha mizigo toka ndani ya gari iliyobeba misaada hiyo.
 Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund kushoto Mohamed Nyongo na Salum Tingwa wakiingia nyumba iliyoathirika na mafuriko kutathmini athari zilizopatikana.
 Wafanyakazi wa Wezesha wakiangalia athari zilizopatikana kwenye mafuriko hayo, ni hali ya hatari kwa kweli watu wengi wamekosa makazi  na wamekosa hata mahali pa kujificha kuweza kuendelea na maisha.  Serikali imewaahidi kuwaandalia eneo la kuwajengea.  Waathirika wanasubiri kama serikali ilivyowahidi.
 Wakinama waathirika wakitoka kuchoka maji mbali sana kutokana na athari ya mafuriko. Waliezea hali halisi ya mafuriko hayo kwamba eneo hilo ni hatari hata kwa kuishi kwani mkondo wa maji umepita tangu miaka mingi iliyopita.

Mto Mkondoa, ni mto ambao umemwaga maji na kusababisha mafuriko baada ya kujaa na kingo za mto kuzidiwa kuhifadhi maji na kuyafanya yatiririke mpaka maeneo wanayoishi watu.  Serikali tunaomba iweze kulifanyia ukarabati daraja hili kwa manufaa ya wananchi wa Kilosa na waathirika kwa ujumla.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »